• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi ya wananchi yaongeza nguvu ya uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2019-10-08 19:42:38

    Katika mapumziko ya wiki moja ya kusherekehea Siku ya Taifa la China, idadi ya matumizi ya watu kwenye sekta nyingi imevunja rekodi, ikiwa ni pamoja na chakula, utalii, filamu na nyinginezo, hali ambayo inaoyesha kuwa matumizi yameendelea kuwa msukumo muhimu zaidi katika kuhimiza maendeleo na ustawi wa uchumi wa China.

    Ustawi wa matumizi ya China unatokana na kuongezeka kwa uwezo wa matumizi ya raia na dhamira yao, pamoja na kuboreshwa kwa ubora wa bidhaa na huduma za makampuni. Ongezeko la mapato ya raia linaimarisha dhamira yao ya matumizi, makampuni ya China yanazidi kufanya uvumbuzi kwa kufuata mahitaji ya mageuzi ya kimuundo kwa upande wa ugavi, na kutoa bidhaa na huduma zenye ubora zaidi.

    Katika miaka ya karibuni, serikali ya China imetunga sera za mfululizo juu ya kulinda utulivu wa maendeleo ya soko. Sera hizo zimesisitiza kuharakisha maendeleo ya sekta za huduma, ikiwa ni pamoja na elimu, matunzo ya utotoni na uzeeni, matibabu, utamaduni, na utalii. Pia kuboresha hali ya mazingira ya matumizi, kukamilisha sera ya kutoza kodi ya mapato kwa watu binafsi ili kuhamasisha matumizi, na kuongeza uwezo wa matumizi.

    Watafiti wa mambo ya uchumi wamesema, matumizi yameendelea kuwa nguvu kuu inayohimiza maendeleo ya uchumi wa China. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, matumizi yamechangia asilimia 60.1 kwa ongezeko la uchumi wa China. Ongezeko la matumizi katika mapumziko ya Siku ya Taifa la China limeonyesha kuwa matumizi ya raia yanatia nguvu kubwa kwa uchumi wa China, hii ndiyo sababu ya uwezo wa uchumi wa China katika kukabiliana na changamoto mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako