• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika Kusini yaendelea kupambana kwa ajili ya amani ya dunia

  (GMT+08:00) 2019-10-09 18:35:46

  Mkurugenzi mtendaji wa Idara ya Uratibu wa Kimataifa iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Uratibu wa Kimataifa nchini Afrika Kusini Bw. Zaheer Laher amesema, nchi hiyo itaendelea kupambana kwa ajili ya amani ya dunia.

  Bw. Laher amesema, Afrika Kusini itaendelea kufanyia kazi kile ilichoanza, hususan kupitia ushirikiano na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, ili kumaliza mapigano na kuchangia katika amani na usalama wa dunia, lengo kuu likiwa ni kuzuia na kusuluhisha migogoro, na kutekeleza maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  Januari mwaka huu, Afrika Kusini ilichukua nafasi yake kama nchi asiye mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako