• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu wanne wauawa katika mlipuko uliotokea pembezoni mwa mji mkuu wa Somalia

  (GMT+08:00) 2019-10-09 18:41:07

  Watu wanne wameuawa na wengine watano kujeruhiwa usiku wa jana baada ya bomu lililotegwa kando ya barabara inayounganisha mji mkuu wa Somalia Mogadishu na mji wa Afgoye katika mkoa wa Lower Shabelle kulipuka.

  Ofisa polisi ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema, bomu hilo lililipuka wakati gari lililobeba askari lilipopita karibu, na kuongeza kuwa askari wawili ni miongoni mwa watu waliouawa.

  Tukio hilo limetokea wakati jeshi la Somalia linafanya operesheni kali ya kuondoa mabomu yaliyotegwa ardhini ambayo wapiganaji wametega katika barabara kati ya Afgooye na Mogadishu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako