• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na viongozi wanaliohudhuria halfa ya kufungwa kwa Maonesho ya kimataifa ya kilimo cha bustani ya China

    (GMT+08:00) 2019-10-09 20:03:33

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi walioshiriki kwenye halfa ya kufungwa kwa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo cha Maua ya China.

    Akikutana na naibu waziri mkuu wa Kyrgyzstan Bw. Kubatbek Boronov, Li Keqiang amesema, China inapenda kuongeza thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili, kukuza ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali haswa uwekezaji, ili kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya.

    Naye Bw. Boronov amesema Kyrgyzstan inazingatia kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati yake na China, pia inapenda kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, na kuongeza ushirikiano katika uwekezaji.

    Katika mazungumzo yake na naibu waziri mkuu wa Azerbaijan Bw. Hajibala Abutalybov, Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa China inapenda kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo ya pamoja.

    Bw. Abutalybov amesisitiza kuwa, Azerbaijan inapenda kuimarisha urafiki na China, na kushiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako