• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Eliud Kipchoge kutimua vumbi Jumamosi kwenye mbio za INEOS 1:59 Challenge

  (GMT+08:00) 2019-10-10 09:10:14

  Eliud Kipchoge anatarajiwa kuwa kivutio cha mabilioni ya wapenzi wa riadha watakaojitokeza katika barabara za jiji la Vienna, Austria na kumfuatilia kwa namna zozote atakapotimua vumbi Jumamosi hii. Bingwa huyu wa Olimpiki na mshika rekodi ya dunia katika mbio za marathon, atapania kuwa binadamu wa kwanza kukamilisha mbio za kilomita 42 chini ya muda wa saa mbili. Ili kufanikisha hatua za mwisho za maandalizi ya Kipchoge, bilionea mmiliki wa kampuni ya INEOS kutoka Uingereza, Sir Jim Ratcliffe aligharimia safari ya ndege ya binafsi aina ya Gulfstream yenye thamani ya Sh bilioni 2.4 za Kenya iliyomfuata mwanariadha huyo nchini siku ya Jumatatu. Kipchoge, 34, alivunja rekodi ya dunia mwaka 2018 kwa kukamilisha kivumbi cha Marathon kwa muda wa saa 2:01:39 nchini Ujerumani. Hata hivyo, nusura rekodi yake hiyo ifutwe na Mwethiopia Keninisa Bekele, 37, aliyekamilisha mbio za Berlin Marathon kwa muda wa saa 2:01:41 nchini Ujerumani mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako