• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Messi asema kashfa ya ukwepaji kodi ilimfanya kutaka kuondoka Barcelona

    (GMT+08:00) 2019-10-10 09:12:25

    Lionel Messi ametamka kwa mara ya kwanza kuwa alitaka kuondoka Barcelona kutokana na sakata la ukwepaji kodi. Nahodha huyo wa Barcelona alisema kitendo cha kudaiwa na Serikali amekwepa kodi ya Pauni 2.95 milioni kilimuweka njiapanda. Messi alipigwa faini ya Pauni 223,000 kwa kosa hilo ambalo alisema lilitaka kuharibu maisha yake Nou Camp mwaka 2017. Hata hivyo, alisema anashukuru kashfa hiyo ya ukwepaji kodi kati ya mwaka 2007 na 2009 ilimpata wakati watoto wake wakiwa na umri mdogo. Mshambuliaji huyo alisema alikuwa na wakati mgumu yeye na familia yake kwa kuwa kashfa hiyo ilikuwa kubwa kwake. Tangu alipojiunga na Barcelona Novemba 2003, amefunga mabao 604 katika mechi 692 alizocheza Barcelona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako