• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais wa China katika Asia Kusini kutoa mchango mpya katika amani na ustawi wa dunia na kikanda

    (GMT+08:00) 2019-10-10 18:22:01

    Kuanzia Oktoba 11 hadi 13 Rais Xi Jinping wa China atakwenda India kuhudhuria mkutano wa pili usio rasmi kati ya viongozi wa nchi hizo mbili na kufanya ziara rasmi nchini Nepal. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Luo Zhaohui amekutana na wanahabari kuzungumzia ziara hiyo na kusema, ziara hiyo ni ya kwanza ya rais Xi baada ya maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya Watu wa China kuanzishwa, pia ni ziara ya kwanza kwa rais wa China nchini Nepal baada ya miaka 23. Ziara hiyo inatarajiwa kutoa nguvu na uhai mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za Asia Kusini, na kuleta fursa mpya ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wenye ufanisi, huku ikijenga jukwaa jipya kwa maelewano na urafiti kati ya watu wa kanda hiyo na kutoa mchango mpya kwa amani na ustawi wa dunia na kikanda.

    China na India zikiwa nchi mbili pekee zenye watu zaidi ya bilioni 1 duniani, ushirikiano kati yao sio tu utasaidia maendeleo ya upande mwingine, bali pia utasaidia kuhimiza dunia yenye ncha nyingi na mchakato wa utandawazi wa uchumi, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea. Tangu mkutano usio rasmi kati ya viongozi wa China na India uliofanyika mwaka jana huko Wuhan, nchi hizo mbili zimesukuma mbele kwa pande zote ushirikiano katika sekta mbalimbali, na migongano husika imedhibitiwa vizuri, na uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Luo Zhaohui anasema,

    "Kwa upande wa kimataifa, wakati hali ikienda kinyume na utandawazi na vitendo vya kujilinda kibiashara vikiongezeka, viongozi wa China na India wanabadilishana maoni, kulinda kithabiti biashara huria na kuhimiza mchakato wa utandawazi wa uchumi. Kutokana na hali ya ndani ya China na India, nchi hizo mbili ziko katika kipindi muhimu cha kuendeleza uchumi na kuimarisha mageuzi. Ni muhimu sana kwa pande hizo mbili kuimarisha mawasiliano ya utawala wa taifa na kutimiza kuunganisha mikakati ya maendeleo. "

    Bw. Luo ameongeza kuwa, katika mkutano usio rasmi, viongozi wa nchi hizo mbili watafanya mawasiliano ya kimkakati kuhusu hali ya kimataifa na uhusiano kati ya pande mbili. Vilevle wanatarajiwa kufikia makubaliano mapya mfululizo, ambayo yatahusu mustakabali wa pamoja kuhusu mageuzi ya mifumo ya kimataifa, majukumu na mchango wa pamoja wa China na India katika mambo ya kikanda, na kutoa maoni ya mwongozo katika mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili, ushirikiano na mawasiliano katika sekta mbalimbali, na kutoa hatua halisi husika. Kutoka mkutano wa Wuhan hadi mazungumzo ya Chennai, viongozi wa nchi hizo mbili wataendelea kuzungumzia mambo ya kimataifa, na wataleta ushawishi mkubwa kwa hali ya kimataifa na kikanda na uhusiano wa kimataifa.

    Nepal ni jirani na rafiki wa China, ambayo pia ni mwenzi muhimu wa China katika kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwenye upande wa Asia Kusini. Katika ziara yake nchini Nepal, rais Xi atahudhuria dhifa ya taifa itakayoandaliwa na rais Vidya Devi Bhandari, pia atafanya mazungumzo na rais Bhandari. Bw. Luo anasema,

    "Viongozi wa nchi hizo mbili watatoa mpango mpya kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Nepal katika siku za baadaye, kuhimiza kuinuliwa kwa kiwango cha uhusiano huo na kufungua enzi mpya ya maendeleo ya kasi ya uhusiano kati ya China na Nepal. Viongozi hao pia watazidisha maelewano ya kisiasa, kuimarisha msingi wa kirafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, na kusisitiza tena kuendelea kuunga mkono upande mwingine katika masuala makubwa na yanayofuatiliwa na pande mbili. Aidha, viongozi hao watahimiza nchi mbili kujenga "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa sifa ya juu, kuharakisha ujenzi wa mitandao ya kuvuka Himalaya, ili kutoa nguvu mpya kwa ushirkiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali na kunufaisha zaidi nchi hizo mbili na watu wao. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako