• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Baadhi ya wadau wa mawasiliano na vyombo vya habari hutumia vifaa vilivyopitwa na wakati

    (GMT+08:00) 2019-10-10 19:15:21

    Ripoti ya mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda imeonesha kuwa baadahi ya kampuni za mawasiliano na vyombo vya habari vinatumia vifaa vilivyopitwa na wakati.

    Mamlaka hiyo imetoa mfano wa tarkilishi ambayo inafaa kutumia kwa miaka 3 lakini Uganda inatumika kwa miaka 4.

    Imesema kuwa matumuizi ya vifaa ambavyo muda wake umepita kunaathiri ubora wa huduma.

    Aidha mamlaka hiyo imedokeza kuwa asilimia 43 ya wadau wa sekta hizo wanafahamu kuwa kuna muda maalum uliowekwa kwa vifaa vya kazi lakini asilimia 57 hawana ufahamu.

    Taakwimu za mamlaka hiyo zinaonesha kuwa vifaa vya mawasiliano vilivyoagizwa kati ya mwaka 2010 na 2017 ni vya gharama ya shilingi trilioni 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako