• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Vyama vya ushirika vya akiba na mkopo zaidi ya 2,000 hatarini kufutwa

    (GMT+08:00) 2019-10-10 19:16:47

    Vyama vya ushirika vya akiba na mkopo zaidi ya 2,000 nchini Tanzania viko hatarini kufutwa kutokana na kutokuwa na anuani jambo ambalo linatia shaka kuanzishwa kwake.

    Hayo yameelezwa na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Tanzania, Tito Haule wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushirika wa akiba na mkopo.

    Amesema vyama vya ushirika kwa sasa vipo 6,137 lakini zaidi ya 2,000 havifanyi kazi ipasavyo.

    Haule amezitaka bodi kuhakikisha sheria za ushirika zinafuatwa, mikutano inafanyika kwa mujibu wa sheria kuhakikisha fedha za vyama vya ushirika zinalindwa.

    Alitoa mfano wa chama cha ushirika kilichofanya vikao 25 kwa mwaka na kila kikao mshiriki analipwa Sh300,000 wakati sheria inasema vikao vifanyike mara nne kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako