• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yafanya opresheni ya kijeshi ya ardhini kaskazini mwa Syria

    (GMT+08:00) 2019-10-10 19:40:11

    Wizara ya ulinzi wa Uturuki jana imesema jeshi lake limefanya opresheni ya kijeshi ya ardhini dhidi ya Kundi la Wakrudi huko kaskazini mwa Syria.

    Shirika la Habari la Syria limesema, raia wanane wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Uturuki kwenye maeneo ya mkoa wa Hasakah, kaskazini mashariki mwa Syria, ikiwa ni pamoja na mji wa Qamishli, al-Darbasiyah, na Ras al-Ayn.

    Akizungumzia shambulizi hilo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inaona siku zote kwamba mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Syria lazima uheshimiwe na kulindwa. Amesema Jumuiya ya kimataifa na pande zote husika zinapaswa kujitahidi kuweka mazingira mazuri katika kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa suala la Syria, na kuepusha hali ya sasa ya Syria kuwa mbaya zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako