• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga serikali ya mji wa Prague wa Czech kuingilia kati mambo ya ndani ya China

    (GMT+08:00) 2019-10-10 19:53:33

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, maofisa wa awamu mpya ya serikali ya Prague, nchini Czech wameingilia kati mambo ya ndani ya China, na kuharibu msingi wa kisiasa wa mawasliano kati ya Prague na Beijing.

    Bw. Geng amesema, tangu mwezi wa Novemba mwaka 2018, maofisa wakuu wa awamu mpya ya serikali ya Prague wamepuuza kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa na makubaliano ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, kutojali msimamo na upinzani wa China, na kutoa hoja zisizofaa kwenye masuala muhimu yanayohusiana na maslahi kuu ya China, na pia kuingilia kati mambo ya ndani ya China. Kutokana na hali hiyo, mji wa Beijing umetangaza kuondoa uhusiano wa mji rafiki na Prague na kusimama mawasiliano yote ya kiserikali kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako