• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashabiki wanawake wa Iran waangalia kwa uhuru mechi ya soka kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi

    (GMT+08:00) 2019-10-11 09:24:47

    Wakiwa wanapeperusha bendera na kujipiga picha za selfi, maelfu ya wanawake wa Iran jana waliangalia mechi ya soka kwa uhuru na ikiwa ni mara ya kwanza katika miongo mingi, baada ya Fifa kutishia kuipiga marufuku nchi hiyo juu ya vizuizi vyake vigumu dhidi ya wanawake kuingia viwanjani. Mashabiki wanawake walivaa bendera ya taifa yenye rangi za kijani, nyeupe na nyekundu kwenye mabega yao na kufunika vichwa vyao huku wakishangilia kwenye uwanja wa Azadi uliopo Tehran ambao unabeba watu laki moja wakiangalia mpambano wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2022 ilipocheza Iran dhidi ya Cambodia. Kwa karibu miaka 40 Jamhuri hiyo ya Kiisalamu imekuwa ikiwazuia mashabiki wanawake kuingia kwenye viwanja vya soka na michezo mingine, kwa hoja ya mashehe kwamba wanawake ni lazima wakingwe na mazingira ya uwepo wa wanaume.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako