• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yamfungia kujihusisha na soka Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda FUFA Moses Magogo

    (GMT+08:00) 2019-10-11 09:25:44

    Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetangaza rasmi kumfungia kujihusisha na soka Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda FUFA Moses Magogo. Awali Magogo alitangaza kujiweka pembeni kwa miezi miwili ili kupisha uchunguzi lakini FIFA imejiridhisha tayari. Baada ya FIFA kujiridhisha kuwa Moses Magogo aliuza tiketi za fainali za Kombe la dunia 2014 kinyume na taratibu, imetangaza rasmi jana kumfungia kwa kipindi cha miezi miwili kujihusisha na masuala yoyote yale ya soka. Kabla ya yote hayo kujiri, Mei 30 2017 mbunge wa jimbo la Makindye Magharibi Allan Ssewanyana alipeleka malalamiko yake FIFA kuwa Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda Moses Magogo aliuza kinyume na taratibu tiketi 177 za Kombe la Dunia 2014 zilizokuwa zimeelekezwa kuuzwa Uganda, Magogo anadaiwa kuuza tiketi hizo nje ya Uganda tofauti na FIFA walivyokuwa wamekusudia kwamba kila shirikisho kuuza tiketi kwa wananchi wa taifa husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako