• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China akutana na viongozi wa biashara wa Marekani na mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)

    (GMT+08:00) 2019-10-11 09:29:58

    Naibu waziri mkuu wa China na mkuu wa upande wa mazungumzo ya China na Marekani Bw. Liu He amekutana na viongozi wa biashara wa Marekani na mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Akikutana na mkuu wa Baraza la Biashara la Marekani na China (USCBC) Bw. Craig Allen, na naibu mtendaji mkuu wa maswala ya kimataifa katika Baraza la Biashara la Marekani Bw. Myron Brilliant, Bw. Liu He amesema uhusiano wa kiuchumi na kibiashara ni muhimu na una athari kwa dunia, na vita ya biashara si nzuri kwa China, Marekani na hata kwa dunia nzima, na kampuni na wateja watapata hasara kubwa.

    Bw. Allen na Bw. Brilliant wamesema hakuna mshindi bali wote wataathiriwa vibaya katika vita ya biashara, na jumuiya ya wafanyabiashara nchini Marekani haitaki kuona nyongeza ya kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako