• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa biashara wa pande nyingi waleta fursa mpya kwa ushirikiano kati ya China na India

    (GMT+08:00) 2019-10-11 18:40:25

    China na India zote ni nchi zinazoendelea na soko linaloibuka, pia ni nchi mbili pekee zenye watu zaidi ya bilioni 1 duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili unazidi kupanuliwa na kuendelea kupata mafanikio makubwa. … ana maelezo zaidi.

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya mambo ya biashara ya China zinaonyesha kuwa, mwaka jana, thamani ya biashara ya pande mbili za China na India ilifikia dola bilioni 95.5 za kimarekani, na kuweka rekodi mpya, ambayo inachukua karibu asilimia 70 ya thamani ya jumla ya biashara kati ya China na sehemu ya Asia Kusini. Naibu mkuu wa idara ya soko la kimataifa iliyo chini ya wizara ya biashara ya China Bw. Bai Ming amesema,

    (Sauti 1)

    "Nchi hizo mbili zinasaidiana sana kiuchumi. Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na India umepata maendeleo dhahiri. Kwa mfano, simu za mkononi za China zinapendwa sana na wateja nchini India. China inahitaji malighafi kadhaa, kwa mfano mawe ya chuma ya India yanauzwa kwa China."

    Takwimu zinaonesha kuwa, China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa India katika miaka kadhaa mfululizo. Bidhaa kuu za China zinazouzwa nchini India ni pamoja na bidhaa za mashine na za kielektroniki, bidhaa za kikemikali, vitambaa na nguo, mashine za kushughulikia data na vifaa vyake, huku bidhaa kuu zinazonunuliwa kutoka India ni pamoja na almasi, bidhaa za mashine na za kielektroniki, vitambaa na nguo na madini ya chuma.

    Wakati huohuo, India pia ni nchi muhimu ya kigeni inayowekezwa na China na soko la ushirikiano la ujenzi wa miundombinu. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa Julai mwaka huu?, makampuni ya China yamewekekza dola bilioni 8.4 za kimarekani nchini India, ambayo inachukua theluthi moja ya uwekezaji wa ujumla wa sehemu ya Asia Kusini. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Agosti, uwekezaji wa India nchini China umefikia dola milioni 920 za kimarekani katika sekta za huduma za software na huduma ya ukusanyaji wa fedha na ukodishaji wa mashine. Akizungumzia fursa za ushirikiano zinazowezekana, Bw. Bai amesema kuwa pande hizo mbili sio tu zinatakiwa kuongeza ushirikiano wa kunufaishana wa kiuchumi na kibiashara, bali pia kuimarisha ushirikiano kupitia mfumo wa biashara ya pande nyingi wa kikanda. Anasema,

    (Sauti 2)

    "China na India zote ni nchi za BRICS. Wakati huohuo, nchi hizo mbili pia ni nchi jirani. Katika hali hiyo, tunatakiwa kuzidisha mawasiliano. Katika mustakabali wa utandawazi wa uchumi, utawala wa dunia katika nchi nyingi duniani unakabiliwa na changamoto mpya. Utaratibu halisi wa ushirikiano kati ya China na India ni uhusiano wa wenzi wa kiuchumi wa pande zote wa kikanda wa "10+6" RCEP. Wakati utandawazi wa uchumi ukigongana na ulinzi wa kiuchumi, tunaweza kutafuta njia mpya ya maendeleo, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaleta nguvu mpya ya maendeleo kwa utandawazi huo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako