• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Vijana laki nane hukosa ajira kila mwaka.

    (GMT+08:00) 2019-10-11 19:02:09

    Vijana wametakiwa kuongeza ujuzi na kuwa wajasiriamali ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine. Hii ni kutokana na ripori kwamba takriban vijana 800,000 kukosa ajira kila mwaka nchini Tanzania.

    Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Asasi ya Anza, inayojishughulisha na ufundishaji vijana masuala ya ujasiriamali na kuboresha mawazo ya biashara, Joshua Silayo.

    Changamoto hiyo imeisukuma Anza na Asasi ya Climate Launch pad kuendesha shindano kwa vijana 10 ili kupata mawazo bora ya biashara, yanayolenga kutunza mazingira yatakayoshindanishwa kidunia.

    Akizungumza wakati wa kutafuta washindi watatu kati ya 10 walioshiriki mafunzo ya masoko, fedha na wateja kwa miezi miwili, Silayo aliyataja malengo yao kuwa ni kukuza ajira tano hadi 10 kwa kila biashara. Alisema washindi watatu waliopatikana watakwenda kushiriki mashindano ya kidunia nchini Amsterdam na kwamba wazo la biashara litakaloshinda litapata Euro 10,000, wa pili Euro 5,000 na wa tatu Euro 2,500.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako