• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza nchi wanachama wa UN kutekeleza wajibu wa fedha

    (GMT+08:00) 2019-10-11 19:17:20

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China inahimiza nchi wanachama wa Umoja huo zitekeleze wajibu wa fedha, ili kutatua matatizo ya fedha yanayoukumba Umoja huo.

    Geng Shuang amesema, kutoa ada kamili ya uanachama wa Umoja wa Mataifa kwa wakati bila ya sharti lolote ni wajibu kwa nchi wanachama katika kutekeleza Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kwamba akiba ya fedha ya kutosha inayoweza kukadiriwa yenye hali ya utulivu ni msingi kwa uendeshaji wa kazi za Umoja wa Mataifa.

    Pia amesema, Marekani ikiwa ni nchi kubwa ya kwanza ya utoaji wa ada hiyo kwenye Umoja huo, haikutoa ada kwa muda mrefu, kiasi ambacho kimefikia dola bilioni 1.055 za kimarekani, hali inayofuatiliwa sana na nchi nyingi.

    Ameongeza kuwa China inatekeleza wajibu wake wa fedha kwa makini kwenye Umoja huo, na kutoa ada zote za uanachama za mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako