• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na waziri mkuu wa India

    (GMT+08:00) 2019-10-12 18:32:19

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Chennai, India alikutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi.

    Rais Xi alipofika Mahabalipuram, jimbo la Tamil Nadu, alikaribishwa na Bw. Modi kwenye mlango wa Mahabalipuram.

    Rais Xi amesema, mwaka jana alikutana na Bw. Modi huko Wuhan, China, na kuongoza uhusiano kati ya China na India kuingia kwenye kipindi kipya. Amesema anafurahi kualikwa kuzuru jimbo la Tamil Nadu, ambalo lina mawasiliano ya muda mrefu ya kihistoria na China, pia ni kituo cha kusafirisha mizigo kwenye njia ya hariri ya zama za kale. Amependekeza pande hizo mbili kutumia fursa ya kuadhimisha miaka 70 tangu China na India zianzishe uhusiano wa kibalozi, kupanua zaidi mawasiliano ya watu, kuhimiza zaidi mawasiliano kati ya ustaarabu tofauti, ili kutia nguvu zaidi kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili na kufanya ustawi mpya wa utamaduni wa Asia.

    Bw. Modi amesema, kutokana na maendeleo ya maelfu ya miaka , India na China zimekuwa makundi mapya muhimu ya kiuchumi duniani, kuimarisha ushirikiano na mawasiliano kuna umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya nchi hizo mbili, pia kutahimiza ustawi wa maendeleo ya dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako