• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Nepal watangaza kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati

    (GMT+08:00) 2019-10-13 17:06:13

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Kathmandu alikutana na rais Bidhya Devi Bhandari wa Nepal, ambapo wametangaza nchi zao kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati, unaoelekea maendeleo na ustawi kwa moyo wa kufanya ushirikiano na kupata maendeleo ya pamoja.

    Rais Xi Jinping amesema China itaendelea kuzidisha mageuzi na kufungua mlango zaidi, ili kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu. Poa amesisitiza kuwa China yenye utulivu, ufunguaji mlango, na ustawi siku zote ni fursa ya Nepal na dunia.

    Rais Bhandari amepongeza maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya watu ya China. Amesema Nepal inapenda kuiga uzoefu wa maendeleo ya China. Pia ameeleza imani kuwa wachina hakika watatimiza ndoto ya ustawi mkubwa wa nchi chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, hali ambayo itasaidia amani, maendeleo na ustawi wa Nepal na kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako