• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi asema ziara ya rais wa China Asia Kusini ni mafanikio mengine ya diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalumu wa China

    (GMT+08:00) 2019-10-14 08:25:54

    Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara katika nchi za Nepal na India kuanzia tarehe 11 hadi 13 mwezi huu, na kuhudhuria mkutano wa pili usio rasmi kati ya viongozi wa China na India.

    Akizungumzia ziara hiyo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema ziara hiyo yenye mafanikio imetia nguvu mpya kwenye uhusiano kati ya China, India na Nepal, kuweka jukwaa jipya la kuhimiza ujirani mwema katika kanda ya Asia Kusini, na kufungua mustakbali mpya wa ushirikiano wa kiutendaji wa kikanda. Amesema ziara hiyo ni mafanikio mengine ya diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalumu wa China.

    Bw. Wang Yi amesema, China inapenda kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana na nchi zote za Asia Kusini. Uhusiano kati ya China na India, uhusiano kati ya China na Pakistan na uhusiano kati ya China na nchi nyingine za Asia Kusini unaweza kuendelezwa kwa pamoja. Amesema uhusiano huo haulengi upande wa tatu, na wala hauathiriwi na upande wa tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako