• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: APR ya Rwanda yawatambia JKT Tanzania nusu fainali Kombe la Nyerere, fainali kuchezwa leo

    (GMT+08:00) 2019-10-14 08:44:35

    Timu ya mpira wa wavu ya wanawake APR kutoka nchini Rwanda imefikia hatua ya fainali ya Michuano ya Kimataifa ya Kombe la Nyerere mwaka 2019 baada ya kuwatambia wenyeji timu ya Jeshi La Kulinda Taifa ya Tanzania kwenye nusu fainali iliyofanyika jana. Michuano hiyo inayoendelea kwa wiki nzima sasa na kukusanya michezo ya aina mbalimbali, inafanyika kila mwaka ili kumuenzi baba wa Taifa la Tanzania Julius Nyerere. Michuano ya mwaka huu inafanyika Arusha. APR, iliyoshinda michuano ya mpira wa wavu kwa wanawake mwaka 2017, ina nafasi ya kutwaa taji leo itakapovaana na timu ya Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai ya Kenya (DCI) katika fainali. Mabingwa watetezi DCI wamejihahakikishia kucheza na APR, jana Jumapili, baada ya kuwazidi nguvu wenzao timu ya Hakika kwa seti (3-0) Katika mchezo wa nusu fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako