• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Taifa ya Tanzania leo inacheza mechi ya kirafiki na Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-10-14 17:04:23

    TIMU ya Taifa Tanzania, 'Taifa Stars', leo itakuwa ugenini kuvaana na wenyeji wao, Rwanda 'Amavubi' , katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Amahoro, Kigali. Mchezo huo ni kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa). Kocha Mkuu wa Tanzania Etienne Ndayiragije anataka kuutumia mchezo huo kujiimarisha kabla ya timu yake kupambana na Sudan katika mchezo wa marudiano kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) utakaochezwa Oktoba 18, Uwanja wa Omdurman, Khartoum. Katika mechi ya kwanza timu ya Tanzania ilifungwa goli 1-0 na Sudan, katika mchezo wa kwanza wa Chan uliochezwa Septemba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mbali ya mazoezi kwa ajili ya kuivaa Sudan, Kocha Ndayiragije anataka kushinda mchezo huo ili Stars ipande katika viwango ya ubora wa soka duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako