• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hakuna mgogoro Shirikisho la Riadha Tanzania- Mwenyekiti

    (GMT+08:00) 2019-10-14 19:29:37

    Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw. Anthony Mtaka amesema hakuna mgogoro unaoendelea kwenye shirikisho hilo. Mtaka amesema hayo wakati akizungumzia kauli ya mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu kukutofanya vizuri katika mashindano ya 17 ya riadha ya Dunia, kuwa kulisababishwa na kutoandaliwa vizuri kutokana na mgogoro ndani ya RT. Simbu alisema timu ya Tanzania iliyoshiriki mashindano ya Doha, Qatar haikupata maandalizi kwa sababu viongozi wa RT walimsusia jukumu hilo Katibu Mkuu wake, Wilhelm Gidabuday. Hata hivyo, Mtaka alikiri kutokuwa na maandalizi mazuri. Alisema Simbu alikuwa na haki ya kuliongelea hilo kutokana na maandalizi yalitopita viongozi, makocha na wachezaji wote kuwa kitu kimoja, lakini sasa walijiweka kando baada ya RT kuandaa kambi Eldoret, Kenya, lakini wanariadha walikataa wakisisitiza kufanya mazoezi Arusha chini ya makocha wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako