• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka nchi za Ulaya zisikilize kwa makini matakwa ya makampuni ya China

    (GMT+08:00) 2019-10-14 19:45:55

    China inazitaka nchi za Ulaya zisikilize kwa makini mapendekezo na matakwa ya makampuni ya China, kuendelea kudumisha uwazi wa soko la uwekezaji, na kuweka mazingira ya biashara yenye usawa, uwazi, utulivu na ya kutabiriwa kwa makampuni ya nchi mbalimbali ikiwemo China yanayowekeza barani Ulaya.

    Shirikisho la Wafanyabiashara la Umoja wa Ulaya nchini China tarehe 11 mijni Brussels lilitoa ripoti likijumuisha biashara kuu zinazofanywa na makampuni ya China huko Ulaya, na kutoa mapendekezo ya sera kwa mashirika ya Umoja wa Ulaya na serikali za nchi wanachama wa Umoja huo, ili kuboresha zaidi mazingira ya biashara ya makampuni ya China huko Umoja wa Ulaya.

    Akizungumzia ripoti hiyo, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema biashara ya makampuni ya China huko Ulaya imeendelea vizuri, na makampuni mengi zaidi ya China yameanzisha vituo vya utafiti na maeneleo (R&D) pamoja na viwanda barani humo. Uwekezaji wa makampuni ya China na ushirikiano kati ya China na Ulaya unahimiza ongezeko la ajira na maendeleo ya maisha ya watu, pia unahimiza kuinuka kwa ngazi ya sekta mbalimbali za Ulaya.

    Ameongeza kuwa China na Ulaya zinatakiwa kushikilia moyo wa kuheshimiana, kusaidiana na kunufaishana, kudumisha kufunguliana mlango na ushirikishi, kuendelea kupanua ushirikiano, hii sio tu inalingana na maslahi ya pande zote mbili, bali pia itaingiza nguvu zaidi chanya na tulivu kwa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako