• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Programu ya utafiti na mafunzo kuhusu ushirikiano wa kisheria ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" yazinduliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2019-10-14 20:15:37

    Programu ya utafiti na mafunzo kuhusu ushirikiano wa kisheria ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imezinduliwa leo mjini Beijing.

    Programu hii ya wiki mbili imeandaliwa na wizara ya mambo ya nje ya China, ni mojawapo ya matokeo makuu ya Kongamano la Pili la Ngazi ya Juu la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Wasomi maarufu watatoa mafunzo na kuwaelezea washiriki kutoka nchi 22 zilizoko kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuhusu masuala mbalimbali ya kisasa juu ya sheria ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani, Shirika la Biashara Duniani, sheria ya uwekezaji ya nchi na mengineyo.Aidha, washiriki hao watatembelea Kasri la Kifalme na Ukuta Mkuu hapa Beijing pamoja na mji wa Chang'an, ambao ni mwanzo wa "Njia ya Hariri ya Kale", ili wajisikie utamaduni wa jadi wa China na "moyo wa Njia ya Hariri".

    Akihutubia ufunguzi wa programu hii, naibu waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Luo Zhaohui, anasema,

    "Njia ya Hariri imewaletea watu biashara, amani na ustawi badala ya dawa za kulevya, ukoloni au vita. Hoja ya "tishio la China" iliyotolewa na baadhi ya nchi kwa makusudi mabaya haina msingi wowote, "Ukoloni Mamboleo" kamwe hautahusiana na China.

    Mshirika kutoka Russia ambaye ni mkuu wa idara ya sheria ya wizara ya mambo ya nje ya Russia Bw. Andrei Metelitsa ana matarajio makubwa kwa shughuli zitakazofanyika kwenye programu hiyo. Anasema,  

    "Natarajia sana kujua utafiti na uzoefu wa China juu ya sheria ya kimataifa, na bila shaka sisi pia tutaelezea maoni na uzoefu wetu. Kwa kuwa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' ni pendekezo lililo wazi lenye ushirikishi, na kila mshiriki anaweza kutoa mchango wake."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako