• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Roger Federer atangaza kushindana kwenye Olimpiki ya Tokyo mwakani

    (GMT+08:00) 2019-10-15 08:47:15

    Roger Federer jana Jumatatu alitangaza kuwa anatarajia kushindana kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo mwakani akiwa katika mbio za kusaka medali ya dhahabu kwa mchezaji mmoja mmoja upande wa wanaume, ikiwa ndio tuzo kubwa ambayo bado hajaipata. Federer ameshinda michuano yote minne ya Grand Slam, na kushinda ATP Tour Finals mara sita, lakini bado anasubiri kuinyakua medali ya dhahabu ya Olimpiki kwa mchezaji mmoja mmoja. Federer ambaye ni bingwa wa Grand Slam mara 20 alishinda medali ya dhahabu kwa wachezaji wawili wawili akiwa na Mswisi mwenzake Stan Wawrinka katika Olimpiki ya Beijing mwaka 2008, lakini aliposhiriki Olimpiki ya London mwaka 2012 kwa mchezaji mmoja mmoja alipata kipigo kikali cha seti 6-2, 6-1, 6-4 kutoka kwa Andy Murray.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako