• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Patriots yaelekea Dar es Salaam kwenye michuano ya kufuzu BAL

    (GMT+08:00) 2019-10-15 08:48:52

    Klabu ya basketball ya Patriots jana iliondoka Kigali kwenda kushiriki michuano ya kufuzu kucheza Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika. Rwanda ipo kundi D na itaanza kampeni zake Oktoba 16 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania. Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji 15, imefanya mazoezi makali kwa wiki nzima katika uwanja wa Amahoro. Katika kundi D Patriots ipo pamoja na Hawassa kutoka Ethiopia, City Oilers ya Uganda, JKT ya Tanzania, Brave Hearts kutoka Malawi, na Dynamo ya Burundi. Muda mfupi kabla ya kuondoka Kocha msaidizi Claude Mukurarinda, amesema wamepangwa kwenye kundi gumu, lakini wanajua mashindano wanayoyakabili na wamejiandaa vilivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako