• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Sababu IAAF kuikataa rekodi ya Kipchoge

    (GMT+08:00) 2019-10-15 16:47:50
    Licha ya Mkenya Eliud Kipchoge kuweka jina lake katika vitabu vya historia upande wa mbio za nyika kufuatia kumaliza kilomita 42 za mbio za marathon kwa saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la INEOS jumamosi nchini Austria, Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) haliitambui rekodi hiyo. Kwa mujibu wa sheria za Shirikisho hilo, ili mbio zozote ziweze kutambulika ni lazima zifikie vigezo ama kanuni zake, jambo ambalo mbio hizo alizoshiriki Kipchoge hazikukidhi vigezo na masharti ya IAAF. Vigezo hivyo ni pamoja na mbio hizo lazima ziwe zimeandaliwa na Shirikisho hilo ama Shirikisho la Riadha la nchi ambapo mbio hizo zinaandaliwa, wanariadha wanaoshiriki hawawezi kuingia na kutoka kwa zamu kama ilivyokuwa katika shindano hilo, na ni lazima kuwa na washindani zaidi ya watatu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako