• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Moshi, Arusha zapokea watalii wengi kutoka Israel

    (GMT+08:00) 2019-10-15 16:53:37
    Miji ya kitalii ya Moshi na Arusha, imeanza kufurika idadi kubwa ya makundi ya watalii kutoka nchini Israel, baada ya serikali kupokea wageni hao zaidi ya 720 waliotua nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

    Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB), Devotha Mdachi, akizungumza juzi usiku, wakati wa kuwapokea watalii hao alisema ujio wa wageni hao ni juhudi kubwa za utangazaji wa vivutio vilivyopo nchini uliofanywa na bodi hiyo kwa kushirikiana na balozi zake.

    Ndege nne zenye watalii kutoka nchini humo ziliwasili katika Uwanja wa Ndege Kimataifa wa KIA uliopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro juzi usiku, zikiwa na maelfu ya watalii.

    Kwa mujibu wa TTB, watalii hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali zikiwamo hifadhi za taifa ili kujionea utajiri huo wa maliasili na baadaye waweze kwenda kushawishi watalii wengine katika nchi zao kuja kujionea wenyewe ni kwa jinsi gani Tanzania isivyosahaulika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako