Mradi huo unalenga kukuza uchumi wa Mkoa wa Dodoma na Taifa kupitia kodi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho, Aliko Mwaiteleke wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina.
Amesema mradi huo upo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake.
Mwaiteleke amesema mpaka sasa upembuzi yakinifu wa mradi huo utakaojengwa kwa njia ya ubia kati ya Hazina Saccos na mwekezaji kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 22 kupitia utaratibu wa Jenga, Endesha na Hamisha (Build, Operate and Transfer - BOT), mwekezaji atagharamia ujenzi wote na kuendesha kwa muda ambao utakubaliwa ndani ya mkataba.
Amesema mradi huo unasimamiwa na Kamati ya watu saba wakiongozwa na Profesa Esta Eshengoma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wajumbe wake kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Bodi ya Manunuzi ya Umma (PSPTB), Kituo Cha Uwekezaji (TIC) na Chuo Kikuu cha Ardhi ambao kwa sasa wanafanya kazi ya kusaka mwekezaji ili kufanikisha mradi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |