• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MASUMBWI: Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo kukipiga na Bondia kutoka kambi ya Manny Pacquiao

    (GMT+08:00) 2019-10-16 09:12:48

    Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo jana alikutana na wanahabari sambamba na kutangazwa kwa mpinzani wake atakayepanda nae ulingoni Novemba 29, ambapo sasa atapambana na bondia Arnel Tinampay kutoka Ufilipino. Bondia atakayepambana nae Mwakinyo anatokea katika kambi ya Manny Pacquiao ni bondia namba 2 nchini Ufilipino baada ya Manny Pacquia hivyo Mwakinyo kwa sasa anapata nafasi ya kupamba na bondia mkubwa ambaye hajawahi kupoteza pambano kwa KO. Pambano hilo litakalochezwa Novemba 29 2019 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, linaweza kuwa pambano la Ubingwa au elimination, ila bado haijathibitika zaidi ya kutangazwa kuwa mapema mwezi Novemba itajulikana. Machi 23 2019 Mwakinyo alimpiga bondia raia wa Argentina Sergio Gonzalez round ya tano kwa TKO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako