• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ronaldo awika huku Ureno ikiteswa mechi ya kusaka tiketi Euro

    (GMT+08:00) 2019-10-16 16:39:55
    Mshambuliaji Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 700 katika taaluma yake ya kucheza soka alipopachika wavuni mkwaju wa penalti dakika ya 72 katika pambano la Euro 2020 ambalo timu yake ya Ureno ilishindwa 2-1 na Ukraine, ugenini. Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 34 ameifungia timu ya taifa mabao 95, mbali na mengine 450 akiwa na Real Madrid, 118 (Manchester United), 32 (Juventus) na matano (Sporting Lisbon). Kichapo hicho cha 2-1, kinamaanisha Ukraine imefuzu kwa fainali hizo za bara Ulaya baada ya kuongoza Kundi B kwa pointi 19 kutokana na mechi saba, kwa mwanya wa pointi nane mbele ya Ureno, ambao wamecheza mechi chache. Ureno ambao wamejikusanyia jumla ya pointi 11 kutokana na mechi sita watacheza na Lithuania na baadaye kumalizana na Luxembourg.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako