• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: TUZO KUU YANUKIA: Gwiji Cheruiyot, Kipchoge katika orodha ya IAAF

    (GMT+08:00) 2019-10-16 16:40:26
    Eliud Kipchoge atakuwa miongoni mwa watimkaji watakaowania taji la Mwanariadha Bora wa Mwaka Duniani kwa upande wa wanaume katika tuzo zitakazotolewa na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) jijini Monaco, Ufaransa mnamo Novemba 23. Kipchoge aliweka historia mnamo Oktoba 12 kwa kuwa binadamu wa kwanza kuwahi kukamilisha mbio za kilomita 42 chini ya muda wa saa mbili aliposhiriki kivumbi cha INEOS 1:59 Challenge jijini Vienna, Austria. Bingwa huyo wa Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika marathon alikamilisha kivumbi cha INEOS 1:59 Challenge baada ya muda wa saa 1:59:40.2. Mkenya mwingine aliyeteuliwa kuwania ufalme wa taji hilo ni Timothy Cheruiyot aliyetwaa nishani ya dhahabu katika mbio za mita 1,500 kwenye Riadha za Dunia zilizoandaliwa majuzi jijini Doha, Qatar. Cheruiyot aliyetawazwa bingwa wa Diamond League mnamo 2017, 2018 na 2019, amewahi pia kunyakua nishani ya fedha katika mbio za mita 1,500 wakati wa Riadha za Dunia zilipoandaliwa jijini London, Uingereza mnamo 2017.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako