• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni muhimu kuhamasisha soko la ndani la kahawa,asema Rais wa Shirikisho la kahawa Uganda,Fred Luzinda.

    (GMT+08:00) 2019-10-16 19:48:22
    Kuanguka kwa bei za kahawa duniani mwaka 2018 kuliwatia wasiwasi wazalishaji wengi wa zao hilo nchini Uganda.

    Uzalishaji mkubwa wa zao hilo hasa kutoka Brazil ulisababisha mavuno mazuri duniani huku nchi hiyo pekee ikizalisha zaidi ya magunia milioni 60.

    Msimu wa 2018/2019 ulisambaza zaidi ya magunia milioni 170 katika soko la kimataifa,ambapo usambazaji uliongezeka kwa magunia milioni 10 zaidi ya mahitaji ya soko,hali iliyosababisha kushuka kwa bei.

    Nchi ya Uganda inazalisha magunia milioni 4 kila mwaka,na kuifanya kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji wa kahawa Afrika baada ya Ethiopia.

    Kulingana na Rais wa Shirikisho la Kahwa Uganda,Fred Luzinda,jumla ya magunia milioni 4.6 ya kilo 60 yalisafirishwa na kuingiza $492 milioni katika mwaka 2018.

    Bei ya wastani kwa kilo ilikuwa $1.84 mwaka 2018 kutoka $1.95 mwaka 2017.

    Hii iliathiri wasafirishaji wa kahawa.

    Luzinda alisema ipo haja kuhamasisha matumizi na ununuzi wa kahawa nchini ili kuwalinda wakulima dhidi ya kuanguka kwa bei katika soko la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako