• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TOKYO 2020: Mbio za Marathon na kutembea kwa kasi zahamishiwa Sapporo kwa hofu ya joto

    (GMT+08:00) 2019-10-17 08:36:18

    Mbio za marathon na kutembea kwa kasi katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo katika majira ya joto zimehamishiwa Sapporo km 800 kaskazini, kwasababu ya hali yake ya baridi. Hatua za kukabiliana na joto katika mji wa Tokyo, zikiwezo kuweka kivuli na kumwagia maji, zimechukuliwa katika michezo ya majaribio ya majira ya joto mwaka huu. Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Thomas Bach amesema ustawi wa wanariadha ndio sababu ya kufanywa mabadiliko hayo. Hali ya hewa ya Sapporo inaweza kushuka kwa nyuzi sita kuliko Tokyo wakati wa majira ya joto. Naye rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mashirikisho ya Riadha Lord Coe amesema kuwapa wanariadha jukwaa zuri la kushindania kwenye mazingira waliyopo ndio kiini cha michezo yote mikubwa, na kuahidi kuwa atashirikiana na waandaaji kuweka mazingira mazuri ya marathan na kutembea kwa kasi katika Michezo ya Olimpiki ya mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako