• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: La Liga yaomba mechi ya Barcelona na Real Madrid kuhamishwa

    (GMT+08:00) 2019-10-17 08:36:45

    Ligi ya Hispania La Liga jana ililiomba Shirikisho la Soka nchini RFEF kuhamishia Madrid mechi inayofuata kati ya Real Madrid na Barcelona itakayochezwa Oktoba 26 kufuatia maandamano ya wafaranikishaji wa Catalonia. Kumekuwa na maandamano kwa siku kadhaa Barcelona baada ya viongozi tisa wa wafarakanishaji wa Catalonia kukamatwa Jumatatu, huku maandamano zaidi yakitarajiwa kufanyika kwenye mji huo siku ya mechi. Hata hivyo Barcelona na Real Madrid hawajahusishwa kwenye ombi la La Liga. Klabu zote mbili zitaulizwa na RFEF kutoa maoni yao, na kamati ya mashindano ya shirikisho itatoa maamuzi katika siku chache zijazo. Jumatatu Shirikisho la Soka la Catalonia lilisimamisha mechi zote mkoani humo, ingawa amri hiyo haihusu mechi za La Liga wala timu ya taifa ya Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako