• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Matumaini ya Taifa Stars kushinda ni madogo itakapovaana na Sudan

    (GMT+08:00) 2019-10-17 08:37:11

    Timu ya Taifa, 'Taifa Stars' ikiwa kesho inajiandaa kwa mchezo wa kimataifa dhidi ya Sudan ambao ni wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika Kwa Wachezaji wa Ndani (Chan), safu ya ushambuliaji inaonekana kusuasua na kuanza kuzima matumaini ya Watanzania kupata ushindi ugenini. Matokeo ya mechi sita za mwisho ilizocheza Taifa Stars hayaipi nafasi timu hiyo kupata ushindi baada ya mchezo wa kwanza kufungwa bao 1-0 na Sudan mjini Dar es Salaam. Timu hiyo ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi katika mechi zote mbili za kufuzu Fainali za Afrika kabla ya kushinda kwa penalti 3-0 ziliporudiana. Pia ilitoka suluhu na Kenya kabla ya kushinda 4-1 katika mchezo wa Chan na kufungwa na Sudan 1-0 na juzi ilitoka suluhu dhidi ya Rwanda. Ubutu wa safu ya ushambuliaji unaonekana kuitafuna Taifa Stars katika mechi zake za mashindano ingawa mara kadhaa Kocha Etienne Ndayiragije alikaririwa akisema atatumia viungo kupata mabao. Kitendo cha kuita idadi kubwa ya wachezaji wa viungo kilionyesha dalili mbaya kwa timu hiyo kupata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako