• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kibadeni : Tanzania tuanze kuwekeza katika vituo vya soka

    (GMT+08:00) 2019-10-17 18:33:23
    Kocha wa zamani wa Simba Abdallah Kibaden amesema kuna haja ya kuwekeza nguvu katika vituo vya soka ili kuandaa wachezaji wa viwango vya juu watakaokuwa msaada kwa timu ya taifa. Kocha huyo amesisitiza hakuna njia ya mkato kulikuza soka la Tanzania kuwa kwenye ushindani wa kimataifa kupitia timu zinazoshiriki Ligi Kuu ama Taifa Stars inapokuwa na majukumu yake. Amesema kama tunatamani kufikia mafanikio ya nchi ambazo zimeendelea kisoka lazima tuangalie misingi yao ipo wapi, asilimia kubwa ya wachezaji wao walijengwa kwenye misingi ya elimu ya soka tangu wakiwa wadogo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako