• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yakishukuru kikosi cha matibabu cha China kwa mchango kiliotolewa nchini humo

  (GMT+08:00) 2019-10-17 19:13:22

  Mjumbe wa waziri wa afya wa Sudan Abdullah Mohamed Ali amekishukuru kikosi cha matibabu cha China kwa kazi zao nchini humo na kusema ushirikiano wa matibabu kati ya China na Sudan umekuwa sehemu muhimu ya ushirikiano wa kina kati ya nchi hizo mbili.

  Aliposhiriki kwenye hafla ya kutunza na kuaga kikosi cha 34 cha matibabu cha China nchini Sudan iliyoandaliwa na balozi wa China nchini Sudan Bw. Ma Xinmin, mjumbe huyu amesema, kikosi hicho kimejitolea bila ya sharti lolote na kusaidia kutoa tiba kwa Wasudan.

  Kwa upande wake, Bw. Ma Xinmin amesema, madaktari 42 wa kikosi hicho wamekabiliana na matatizo ya tofauti ya hali ya hewa na mazingira, kizuizi cha lugha na ukosefu wa vifaa vya tiba, na kushirikiana na madaktari wa Sudan kutoa matibabu bure kwa wagonjwa elfu 71 na kufanya upasuaji mara elfu 4.2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako