• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya Umoja wa Ulaya yafikia makubaliano na serikali ya Uingereza kuhusu BREXIT

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:21:20

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker ametangaza kuwa, kamati hiyo imefikia makubaliano na serikali ya Uingereza kuhusu Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo.

    Bw. Juncker amesema makubaliano hayo yenye usawa na uwiano mzuri yamethibitisha kuwa wametimiza ahadi ya kutafuta utatuzi wa suala hilo. Pia Bw. Juncker amewashauri viongozi kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya kuunga mkono makubaliano hayo wakati wa mkutano wa siku mbili wa Umoja huo uliofanyika leo mjini Brussels.

    Habari zinasema, makubaliano hayo yanapaswa kupitishwa na bunge la Ulaya na bunge la Uingereza kabla ya kuanza kutekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako