• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda- Tume ya Mawasiliano Uganda (UCC) yapendekeza udhibiti wa mitandao ya kijamii

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:43:52

    Tume ya Mawasiliano Uganda (UCC) inapendekeza udhibiti wa huduma za mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter ili kuhimiza uwekezaji katika sekta hiyo.

    Katika mkutano ulioandaliwa na UCC,ambao ulivutia wadau kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika sekta ya mawasiliano,Tume hiyo ilipendekeza kuwa nchi za Afrika zisimame imara katika kushughulikia masuala ya huduma za mitandao ya kijamii.

    Mbali na hayo,pendekezo hilo lilisema kuwa mapato ya mitandao sio imara dhidi ya wahudumu wa mitandao ya simu na watoa huduma za miundombinu ambayo mitandao hiyo inastawi.

    Mkurugenzi wa uhandisi na miundombinu ya mawasiliano katika Tume ya mawasilian Uganda, UCC ,Bi.Irene Kaggwa,alisema usawa unafaa kuwekwa kati ya watoa huduma za mitandao ya simu na watoa miundombinu ili kuimarisha ushindani kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako