• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanyarwanda wawili wateuliwa fainali ya Africa Netprenuer Prize Initiative (ANPI)

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:44:12
    Africa Netpreneur Prize Initiative (ANPI) imetoa majina ya watu 10 walioingia fainali ya shindano hilo,ambapo mshindi atatangazwa tarehe 16 Novemba jijini Accra,Ghana.

    Wanyarwanda wawili ni miongoni mwa wajasiriamali walioteuliwa.

    Wanyarwanda hao ni mwanzilishi wa kampuni ya viatu ya UZURI KY,Kevine Kagirimpundu na Christelle Kwizera,mwanzilishi wa Water Access Rwanda ambayo ilianzisha mradi wa kuvitengeza visima vilivyoharibika na kuvifanya kuwa vibanda vya kisasa vya maji vinavyotumia umeme wa jua.

    ANPI ni mpango wa uhisani unaoongozwa na Wakfu wa Jack Ma,ambao unalenga kuwasaidia kuhamasisha kizazi kijacho cha wajasiriamali wa Afrika.

    Washindi watapokea zawadi ya $1 million.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako