• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dodoma,Tanzania-Wafanyabiashara waonywa kutoapnga biashara kwenye njia za watembea kwa miguu

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:44:27
    Wafanyabiashara jijini Dodoma wametakiwa kuacha kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi,yakiwamo yanayotumiwa na watembea kwa miguu.

    Ofisa masoko wa jiji hilo,James Yuna,aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara na wachuuzi kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutumia maeneo hayo.

    Yuna aliwataka wafanyabiashara hao kutokuwa chanzo cha mgogoro kati yao na halmashauri kwa kukiuka kanuni na taratibu walizowekewa za kutofanya biashara katika maeneo hayo.

    Ofisa huyo alisema wafanyabiashara wanapanga biashara hadi kwenye njia za watembea kwa miguu kando ya barabara,hali inayohatarisha usalama wao pia.

    Kwa upande wao,wafanayabiashara wanaojishughulisha na kufanya biashara mitaani na pembezoni mwa barabara ,kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo,walisema wanalazimika kupanga bidhaa kwenye maeneo yasiyo rasmi kutokana na kukosa nafasi maeneo yaliyotengwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako