• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Japan kuheshimu ahadi ya kukumbuka historia ya uvamizi

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:45:23

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema, China imeitaka Japan kuheshimu ahadi yake ya kukumbuka na kuikubali historia yake ya uvamizi.

    Kauli hiyo imekuja baada ya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kupeleka sadaka katika hekalu la Yasukuni, na baadhi ya mawaziri na wabunge wa nchi hiyo kwenda kutoa heshima zao katika hekalu hilo mapema leo.

    Geng Shuang amesema, China imewasilisha malalamiko makali kwa Japan, na kuongeza kuwa China inafuatilia hatua hiyo hasi kutoka Japan inayohusiana na hekalu la Yasukuni.

    Amesema hatua ya baadhi ya wanasiasa wa Japan inaonyesha tena mtazamo wao mbaya dhidi ya historia ya uvamizi, na kuitaka Japan kuchukua hatua halisi za kivitendo ili kuweza kuaminiwa na nchi jirani zake na jamii ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako