• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakaribisha makampuni ya nchi za nje ikiwemo Marekani kuongeza ushirikiano wa uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-10-17 20:42:36

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amesema, China itafungua mlango zaidi, na kukaribisha makampuni ya nchi za nje ikiwemo Marekani kuongeza ushirikiano na China katika sekta ya uwekezaji, ili kutimiza mafanikio ya pamoja.

    Bw. Li ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa Marekani ulioongozwa na mwenyekiti wa bodi ya kamati kuu ya biashara kati ya Marekani na China Evan Greenberg. Amesema China imefungua sekta ya uzalishaji kwa pande zote, na inafungua sekta ya huduma, na kuongeza kuwa, China ni nchi yenye watu karibu bilioni 1.4, na fursa yake ya maendeleo pia ni kwa dunia nzima.

    Bw. Li amesisitiza kuwa China na Marekani zinapaswa kutatua msuala kwa mazungumzo yenye usawa na kuheshimiana, na amewataka wafanyabiashara na wanaviwanda wa Marekani kuendelea kuchangia maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo, na maelewano kati ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako