• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: David de Gea na Paul Pogba kukosa mchezo wao dhidi ya Liverpool

    (GMT+08:00) 2019-10-18 08:40:49

    Manchester United itawakosa nyota wake David de Gea na Paul Pogba katika mchezo wao muhimu dhidi ya Liverpool utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Old Trafford. De Gea ameongeza orodha ya majeruhi United baada ya kuumia nyonga wakati akichezea Hispania katika mchezo wa kufuzu kwa Euro 2020 dhidi ya Sweden. Man United pia itamkosa kiungo wake Pogba ambaye bado anauguza majeraha ya kifundo cha mguu akiwa amecheza mechi mbili tu tangu Agosti. Mfaransa huyo amereja Dubai katika hali ya hewa ya joto kuendelea na matibabu ya mguu huo yatakayomweka nje hadi mwisho wa mwezi huo. Man United inatumaini nyota wake kadhaa waliokuwa majeruhi watarejea mapema kabla ya mchezo huo wa Jumapili, lakini Luke Shaw, Jesse Lingard na Diogo Dalot bado hali zao hazijatengemaa. .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako