• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NETIBOLI: Ukata wafanya kambi ya Taifa Queens kuvunjwa na Tanzania kujitoa mashindano Afrika

    (GMT+08:00) 2019-10-18 08:41:32

    Wakati mashindano ya Netiboli Afrika yakitarajiwa kuanza leo Ijumaa huko Afrika Kusini, Chama cha Netboli Tanzania (Chaneta) kimevunja kambi ya timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Queens' rasmi jana kufuatia timu hiyo kujiondoa kushiriki kutokana na ukata. Wachezaji wa Taifa Queens walipewa taarifa za kutoshiriki mashindano hayo usiku wa kuamkia Alhamis Agosti 17 na kila mmoja kutakiwa kurejea nyumbani. Tanzania ilipangwa Kundi A na timu ya Uganda, Zimbabwe na Kenya katika mashindano hayo yanayoshirikisha Malawi, Afrika Kusini, Zambia na Lesotho. Uongozi wa Chaneta tayari ulikuwa umelipia ada ya ushiriki dola 550 umelazimika kuvunja kambi hiyo iliyokuwa ikifanyika Keko, Dar es Salaam na jana Alhamisi Alfajiri wachezaji wakaondoka kurudi nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako