• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Patriots yaisomesha namba Dynamo kwenye mashindano ya kufuzu Ligi ya Basketball Africa

    (GMT+08:00) 2019-10-18 08:42:05

    Timu ya Patriots ya Rwanda imeanza kampenzi zake za kujikatia tiketi ya Ligi ya Basketball Africa mwaka 2020 (BAL) kwa ushindi baada ya jana kuwagaragaraza Mabingwa wa Burundi Dynamo, kwenye mashindano ya kufuzu ambayo yameanza juzi Jumatano na kuendelea hadi Jumapili katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Tanzania. Timu hizo mbili zipo kundi D pamoja na timu nyingine tatu. Katika mechi iliyoendelea kwa karibu saa 4 kutokana na mvua kubwa na kukatika kwa umeme, Patriots waliweza kuchukua ushindi kwa kupachika vikapu 73-64. Baada ya mechi yao hii ya ufunguzi Patriots watarejea tena kiwanjani leo na kuvaana na Hawassa ya Ethiopia kabla ya kuja kuwakabili wenyeji JKT kesho Jumamosi. Mabingwa hawa wa Rwanda watamaliza kampeni yao dhidi ya City Oilers siku ya Jumapili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako