• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Cheche awaondoa hofu Azam

    (GMT+08:00) 2019-10-18 16:38:34
    Kocha msaidizi wa Azam, Iddi Nassor 'Cheche', amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo baada ya kusema kikosi chao kipo tayari kwa kupambana wakati wowote. Azam wanatarajiwa kuvaana na Simba Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Cheche amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita. Cheche alisema wanaendelea kujifua katika uwanja wao wa Azam Complex, Dar es Salaam ili kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu dhidi ya Simba.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako