• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar Aiways yazindua safari ya ziada kutoka Doha hadi Mombasa

    (GMT+08:00) 2019-10-18 17:16:25

    Idadi ya watalii nchini inatarajiwa kuongezeka hii ikiwa ni baada ya shirika la Qatar Airways kuzindua safari ya ziada kutoka Doha kwenda Mombasa.

    Safari hii inafikisha tano idadi ya safari za kila wiki katika jiji la Mombasa kutoka Doha na inatarajiwa kuwaleta watalii wakati wa msimu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya. Safari hiyo inatarajiwa kuanza Desemba 20, 2019, hadi Machi 27, 2020.

    Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Akbar Al Baker alisema kuwa kuzinduliwa kwa safari hiyo ni mojawapo ya njia zitakazosaidia katika kudumisha uhusiano kati ya Kenya na Qatar na kutasaidia katika kuongeza nafasi za kazi katika maeneo ya Pwani mwa Kenya.

    Aliongeza kuwa shirika la Qatar Airways litahudumu safari hiyo ya ziada kwa kutumia ndege aina ya Airbus A320 ambayo ina viti 12 katika sehemu ya abiria wa kiwango cha business class na viti 120 katika sehemu ya economy class.

    Pwani mwa Kenya kuna vivutio vingi vya watalii hasa Old Town, Fort Jesus, Haller Park na Mbuga ya Kitaifa ya Mombasa Marine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako